Psalms 135

Wimbo Wa Sifa Kwa Mungu


1 aMsifuni Bwana.

Lisifuni jina la Bwana,
msifuni, enyi watumishi wa Bwana,

2 bninyi ambao mnatumika ndani ya nyumba ya Bwana,
katika nyua za nyumba ya Mungu wetu.


3 cMsifuni Bwana, kwa kuwa Bwana ni mwema,
liimbieni sifa jina lake, kwa maana hilo lapendeza.

4 dKwa maana Bwana amemchagua Yakobo kuwa wake mwenyewe,
Israeli kuwa mali yake ya thamani.


5 eNinajua ya kuwa Bwana ni mkuu,
kwamba Bwana wetu ni mkuu kuliko miungu yote.

6 f Bwana hufanya lolote apendalo,
mbinguni na duniani,
katika bahari na vilindi vyake vyote.

7 gHufanya mawingu kupanda kutoka miisho ya dunia;
hupeleka umeme wa radi pamoja na mvua
na huleta upepo kutoka ghala zake.


8 hAlimuua mzaliwa wa kwanza wa Misri,
mzaliwa wa kwanza wa wanadamu na wanyama.

9 iAlipeleka ishara zake na maajabu katikati yako, ee Misri,
dhidi ya Farao na watumishi wake wote.

10 jAliyapiga mataifa mengi,
na akaua wafalme wenye nguvu:

11 kMfalme Sihoni na Waamori,
Ogu mfalme wa Bashani
na wafalme wote wa Kanaani:

12 lakatoa nchi yao kuwa urithi,
urithi kwa watu wake Israeli.


13 mEe Bwana, jina lako ladumu milele,
kumbukumbu za fahari zako, Ee Bwana, kwa vizazi vyote.

14 nMaana Bwana atawathibitisha watu wake,
na kuwahurumia watumishi wake.


15 oSanamu za mataifa ni fedha na dhahabu,
zilizotengenezwa kwa mikono ya wanadamu.

16 pZina vinywa, lakini haziwezi kusema,
zina macho, lakini haziwezi kuona;

17 qzina masikio, lakini haziwezi kusikia,
wala hakuna pumzi katika vinywa vyao.

18 Wale wanaozitengeneza watafanana nazo,
vivyo hivyo wale wote wanaozitumainia.


19 rEe nyumba ya Israeli, msifuni Bwana;
ee nyumba ya Haruni, msifuni Bwana;

20 ee nyumba ya Lawi, msifuni Bwana;
ninyi mnaomcha, msifuni Bwana.

21 sMsifuni Bwana kutoka Sayuni,
msifuni yeye aishiye Yerusalemu.

Msifuni Bwana.
Copyright information for SwhKC